JACKLINE WOLPER AMUENZI KANUMBA KIPEKEE


MSANII wa filamu nchini Jacqueline”Jackie” Wolper amuenzi marehemu Steven Kanumba kivingine kwa kutoa filamu ya ‘After Death’ ambayo ni mwendelezo wa filamu iliyochezwa na marehemu Steven Kanumba ikiwa ni moja ya kuviendeleza vipaji alivyoacha marehemu Kanumba

Filamu hiyo ambayo pia imezinduliwa siku ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja tangu Kanumba afariki April 7 katika viwanja vya Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya kuviendeleza vipaji vya watoto waliocheza na marehemu katika filamu ya Uncle JJ wanaojulikana kwa jina la Patrick na Jenifer

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Wolper alisema kuwa filamu hiyo aliiandaa katika mazingira maalumu kwa ajili ya kumuenzi Kanumba ambaye kila mtanzania anatambua mchango wake kukuza sanaa kiujumla

Alisema kuwa ameamua kumuenzi kwa kutoa filamu hiyo ya muendelezo wa filamu ya Uncle JJ na kucheza na watoto hao ili kuhakikisha anamuenzi kwa vitendo huku akimuombea alale mahali pema peponi

"Filamu ya Uncle JJ ni filamu ambayo yeye mwenye Kanumba alikuwa anaipenda na kuikubali sana hivyo kumuenzi kwa vitendo ni moja ya ya kukamilisha dhamira yake ambayo amejiwekea" alisema Wolper