Huyo ndo Senetor Nairobi Almaarufu "Sonko"

Seneta wa Jimbo la Nairobi, Gideon Mbuvi ‘Sonko’.
 MBUNGE ‘sharobaro’ anayependwa na wengi na anayejichanganya sana na watu wa kipato cha chini, Gideon Mbuvi ‘Sonko’ ametangazwa mshindi wa kiti cha Useneta wa Jimbo la Nairobi, Kenya.


Wakati akitangazwa kuwa mshindi, Sonko alikuwa kapiga bonge la t-shirt ya njano, kofia na hereni huku kwenye mkono akiwa ametupia pete kadhaa za gold pamoja na saa kubwa mkono wa kushoto.
Sonko ambaye amepata umaarufu kwa usharobaro wake ambao ulimfanya kuwa mbunge wa kwanza kwenye historia ya Kenya kuingia bungeni akiwa amevaa hereni, ameshinda kwa kupata kura zaidi ya laki nane wakati mpinzani wake Wanjiru alipata kura laki tano. Katika uchaguzi huo kwa nafasi ya urais, Uhuru Kenyatta ndiye aliibuka kidedea.