MAGOROFA YOTE DSM KUPIGWA RANGI MOJA...tetesi!



JAMANI, kuna jamaa yangu kaniambia kuwa kuna mpango wa kutunga sheria ndogondogo za jiji la dsm ambazo zitawalazimisha wamiliki wa magofora hasa yale residential (ukiondoa yale mapya ya maofisi), KUPIGWA RANGI YA AINA MOJA ikiwa ni mbinu mojawapo ya kulipendezesha jiji la DSM kabla mabasi ya mwendo kasi hayajaanza.

Nilifurahi kusikia hivyo, kwasababu ukiangalia kwamfano kariakoo, kuna magorofa machafuuuu, just when you are approaching fire ukitokea magomeni angalia kwa mbele uone picha ya magorofa ya kibongo yalivyo, yana rangi mbaya, mengine mekundu, mengine ya kijani, mengine kama yanataka kudondoka, mengine yamezeeka, mengine njano mengine ya kijivu, yaani hata uzuri wa jiji hauuoni.....DO YO THINK THIS CAN WORK, NA HAO WAMILIKI WATAKUBALI KUGARAMIA GARAMA HIZO KWELI?

magorofa ya ulaya, hata kama sio mapya sana, lakini utakuta mengi yanafanana rangi, na ukifika tu unaona jiji linavutia, sio unafika unaona jiji kama umefika chochoro za INDIA au bangladesh...