MAKUBWA YAMKUTA ISHA RAMADHANI,AFANYIWA MCHEZO KARIAKOO...ATAFUTIWA SKENDO
12:34
MAKUBWA
YAMKUTA ISHA MASHAUZI, 'ABAMBIKIZIWA' KESI YA WIZI
Asota
Msimbazi Polisi jana usiku kwa masaa matatu
MKURUGENZI
wa Mashauzi
Classic, Isha Ramadhani Mashauzi jana alionja adha ya
umaarufu baada ya kusoteshwa kituo
cha polisi cha Msimbazi huku kamera za
waandishi maarufu zikimsubiri nje ya kituo hicho.
Isha alifikishwa kituoni
hapo kwa
kuhusishwa na upotevu wa shilingi
laki saba uliotokea kwenye duka moja la Kariakoo
jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa duka hilo la nywele,
amemfikisha Isha na mwenzake aitwae
Halima kituoni hapo akidai alipotelewa na kiasi hicho
cha pesa huku msanii huyo akiwa
ni wa mwisho
kuingia dukani mwake.
Saluti5 ilifika
kituoni hapo majira ya 5 za
usiku na
kukuta waandishi wengi wakimsubiri Isha atoke ili
wapate picha, jambo ambalo walifanikiwa
licha ya Isha kujitahidi kuwakwepa.
Inaaminika mmiliki wa duka hilo
alipiga simu karibu kwa kila
chombo cha habari ili waandishi wafike
hapo akiamini kuwa jambo hilo
litasaidia kumdhalilisha msanii huyo.
Akiongea na Saluti5 muda mfupi baada
ya kutoka kituoni hapo, Isha
alisema alifika dukani kwa dada huyo Jumamosi iliyopita
lakini baada ya kukosa alichokifuata
aliingia duka lingine na kuliacha
gari lake jirani na duka hilo.
Wakati anarudi kwenye gari lake,
wafanyakazi wawili wa duka hilo
wakamfuta na kumwambia kuna upotevu wa pesa
umetokea.
Isha anasema baada ya mjadala wa
muda mrefu akaawachia namba ya simu
na kuwaambia iwapo bado watahitaji
ufafanuzi zaidi wawasiliane.
Isha anasema: Kuanzia
Jumatatu alianza kunipigia simu za vitisho na
kuniambia atanikomesha na kunidhalilisha.
Vitisho
vilipokithiri, Jumanne jioni nikaenda kituo cha Msimbazi kuripoti juu ya
vitisho vyake, lakini kituoni wakaninyima ushirikiano wakaniambia niende Kinondoni ninakoishi.
ŇNikawaambia
nimekuja Msimbazi kwa vile biashara
ya mtu anayenipa
vitisho hivyo ipo Kariakoo, lakini
bado walikataa kunihudumia.
ŇNilirudi
nyumbani nikipanga kuwa kesho yake
niende kituo cha Oysterbay lakini leo (jana)
nikapigiwa simu kutoka Msimbazi kuwa nifike kituoni
hapo.
ŇNikadhani
labda sasa wameamua kunisikiliza, nilipofika kituoni hapo nikawekwa chini ya ulinzi
kwa tuhuhuma
za wizi wa
shilingi laki 7.Ó
Baada ya kusota kwa masaa
kadhaa Isha aliruhusiwa lakini akitakiwa kurudi tena kituoni hapo
siku inayofuata (le0).
Watu kadhaa walifika kituoni hapo kumwekea
dhamana Isha ambaye aligoma kabisa kuingizwa mahabusu.
Waliofika hapo akiwepo mtangazaji wa
Times FM, Dida walifikia hata hatua ya
kutaka kulipa pesa hizo lakini
Isha alikataa kabisa jambo hilo
lisifanyike akidai hii ni aina
mpya ya utapeli.
Haiwezekani
duka ambalo lina wafanyakazi wawili na wateja
wengi wanaoingia useme mtu fulani
kakuibia.
Kwanza mteja
unakuwa nyuma ya kaunta yao na si
rahi kujua pesa zilipo, utalivuka
vipi hilo kaunta mpaka ufike
kwenye pesa bila wahusika kukuona?
Kwanini wasinikamate muda huo huo
na kunipigia kelele za mwizi?Ó
alihoji Isha.
Askari mmoja wa
kituo hicho aliiambia Saluti5 kuwa malalamiko ya kesi
hiyo yana mushkel na yamekaaa
kiujanja ujanja ujanja.
Ameshangaa ni kwanini tukio la Jumamosi liachiwe hadi Jumatano, akashaangaa pia namna waandishi walivyotaarifiwa tukio hilo ndani ya
muda mfupi.
Chanzo:saluti5.com

0 comments:
Post a Comment