Mh. Lowassa atoa msaada wa sh. mil. 5 kwa Baraza la Misikiti Tanzania

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi msaada wa shilingi mil. 5 kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Sheikh Salum Sung'he kwa ajili ya kuendeleza mipango kazi wa BAMITA katika kutoa Elimu kwa Jamii juu ya kupunguza maambukizi ya Ukimwi na Kudhibiti Mimba kabla ya Ndoa.Makabidhiano hayo yamefanyika leo jijini Dar es Salaam.Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA),Alhaj Juma Swalehe.