MTUMISHI WA WIZARA YA ELIMU ANASWA AKIWA GESTI NA MUME WA MTU
02:01
Kapu la habari lililosheheni picha za video liliwasilishwa mbele ya
gazeti moja maarufu hapa nchini hivi karibuni na mwanamke mmoja
aliyejitambulisha kwa jina la Sarah huku maelezo yakimtuhumu Rose
kujivinjari na mumewe katika faragha haramu.
Habari
zilieleza kwamba, mtumishi huyo wa wizara alidaiwa kuingilia ndoa
ya mtu kwa kutumia safari zake za kikazi kula nyama ya ulimi na mume wa
mtu huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kesi ambaye hatimaye alinaswa
naye.
“Kuna
watu waliniambia kuwa, Kesi ambaye ni mume wangu anatembea na mwanamke
huyo, nikaanza kufuatilia hatua kwa hatua kwa kuwatumia watu wakiwemo
watumishi wa hoteli aliyofikia Rose na mume wangu.
“Sikupenda
kuwaingilia chumbani na kuwaharibia starehe zao, nilichotaka mimi ni
ushahidi, nilitumia ujanja wangu kupenyeza kamera nikapata picha,” alisema Sarah huku akifungua kompyuta mpakato yake (laptop) na kuonesha tukio zima mbele ya ofisi ya gazeti hilo.
Katika kulithibitisha tukio,mtumishi huyu wa Wizara ya Elimu alipigiwa simu na maongezi yakawa kama ifuatavyo
Mwandishi: Habari yako dada Rose?
Rose: Nzuri, naongea na nani?
Mwandishi: Naitwa (tunalihifadhi) ni mwandishi wa Gazeti la Ijumaa.
Rose: Ndiyo, unasemaje?
Mwandishi: Aaa, hapa kuna tuhuma zako kwamba unatembea na mume wa mtu na kwamba hivi karibuni ulikuwa naye ndani ya gesti moja mjini Morogoro, lakini pia zipo picha za video na mnato zikionesha mambo machafu mliyoyafanya huko, sijui unajua chochote kuhusu hili?
Rose: We uko wapi, …kama ni ofisini nakuja sasa hivi kuziona hizo picha, nitakujibu nikifika.
Bila kuchelewa, dakika 27 baadaye Rose alifika katika ofisi za Ijumaa akiwa na mumewe na waliomba kuziona picha, jambo ambalo liliwapa wakati mgumu wahariri kukubali zoezi hilo lifanyike mbele ya mwanaume huyo.
“Sikiliza kijana, huyu ni mke wangu, sasa unataka kuficha nini, umempigia simu, kaniambia, sisi tukakubaliana tuje wote kama mwili mmoja, sasa wewe unakataa nini…au ulikuwa na mambo yako?” alihoji kwa ukali mume wa mwanamke huyo.
Wahariri hatimaye walikubaliana na ombi la wanandoa hao kuona picha hizo kwa pamoja, hivyo walipelekwa kwenye kompyuta na kuanza kufunguliwa kifurushi kimoja baada ya kingine .
“Mume wangu tulikuwa tumekaa tu hapa, huyu kaka alikuja kunitembelea chumbani, umeona nimevua nguo?” Rose alijitetea kwa mumewe baada ya kifurushi cha kwanza kufunguliwa na kuwaonesha wakiwa wamekaa kitandani na jamaa.
Kauli hiyo ya mtumishi huyo wa umma mbele ya mumewe ilikuwa kama kutia nazi kwenye supu kwani kimsingi video iliwaonesha wawili hao wakishirikiana ipasavyo hali iliyomfanya mumewe ashushe pumzi.
Mpaka mwisho wa sinema hiyo yenye dakika chache lakini zenye ‘machungu’, wanandoa hao waliondoka wakiwa ‘wamelowa’ jasho
HABARI HII IMEANDALIWA KWA HISANI YA MAGAZETI PENDWA YA GLOBAL PUBLISHER .JIPATIE NAKALA YAKO LEO
0 comments:
Post a Comment