Sakata La Msanii Wa Bongo Movie Kulewa Hadi Kuvua Nguo[Picha]




Isabela "Vai wa akiwa chakali kwa mitungi

Hisia zetu zinatupeleka pabaya sasa na kuacha fikra zetu ziamini kuwa msanii huyu anapenda hali hali hii kwani hafanyi tukio lolote baya kama hakuna waandishi wa habari ,hali hii imefanya jamii isimuelewe na hata wasanii wenzie wameanza kumtilia shaka na kusema anaichafua tasnia ya filamu nnchini kwakulitumia vibaya jina la bongo movie kila anapohojowa au kuwa maeneo ya waandishi hujinadi kama msanii wa bongo movie.

Akizungumza na mtandao huu raisi wa shirikisho hilo nchini bwana Saimoni Mwakifwamba amesema wanasikitishwa na watu wa aina hiyo na kusema wamepanga adhabu kali sana kwa wale wote watakaofanya matukio ya kijinga na kuichafulia sifa swahili hood ambayo imeanza kukuwa na kutowa ajira kwa kwa watu wengi sana.

Nadhani tutakumbuka kuwa si mara ya kwanza kwa msanii huyu kuvuma na kuchukuwa sura katika kurasa za magazet na blog mbali mbali kwa tabia yake ya kuvua nguo,tabia ambayo mwanzo watu walidhani ni bahati mbaya lakini kwa sasa inakuwa kila kukicha.