'Unenguaji si Umalaya, ni kama kazi zingine tu' - Mama Nzawisa

WANENGUAJI wa bendi ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma (BABA YA MUZIKI) Amina Said (Queen) na Kinacho Said (Mama Nzawisa) wamesema kuwa wengi wa mashabiki wanaowaona jukwaani wanawafikiria kuwa wao ni malaya jambo ambalo si la kweli.