Zitto Kwabwe Aikana Number yake ya Simu Baada ya Kutajwa Kwenye Tamko la Njama za Kuiua Chadema




Zitto Kabwe Ameandika Haya Kwenye Account yake ya Facebook Baada ya Number yake kutajwa katika tamko la Chadema lilitoka jana kuhusu njama za kuiuwa Chadema....Haya ndio aliyoandika:

"Namba hiyo iliyotajwa katika TAMKO imewahi kuwa namba yangu ya Simu. Namba hii nimeacha kuitumia toka mwezi Juni/Julai mwaka 2012. Hata hivyo namba hii bado inaonekana kwenye businesscard yangu na kwenye email zangu sehemu ya anuani. Namba hii haijawahi kuwa ya Zoka. Imewahi kuwa ya Zitto Zuberi Kabwe peke yake. Namba hii haitumiki toka katikati ya mwaka 2012.
Kama JF inataka kuthibitisha hili waunde jopo la wanaJF watakaopata taarifa za namba hii popote wanapoweza kupata.

Mambo 2, 
ama namba hii imewekwa kwa bahati mbaya kwenye tamko tajwa au 

imewekwa makusudi kwa sababu maalumu zenye lengo la kutoa ujumbe fulani kwa watu. 

Kwa namna namba hii ilivyochomekwa kwenye tamko hili au hapa JF au vyote kwa pamoja, ni dhahiri kuna juhudi za kunihusisha na upuuzi huu wa ugaidi na unyama dhidi ya binaadamu.

Napenda kusisitiza kwamba, sihusiki kwa namna yeyote ile katika kuwaza, kupanga au kutekeleza mipango yeyote ya kudhuru mtu ama kwa njia za kigaidi au za kijinai. Sihusiki kwa namna yeyote ile kupanga mpango wowote ule wenye lengo la kuhusisha chama changu na vitendo vyovyote vya kigaidi au kudhuru mtu yeyote yule. Juhudi zozote zinazofanywa na maadui wa chama changu za kunihusisha na mambo haya zitashindwa kwani siku zote ukweli huwa bayana.
Napenda kuweka wazi kwamba Mhariri wa Mwananchi ndugu Dennis Msacky ni rafiki yangu wa karibu sana. Ninaamini kabisa kwamba katika suala hili Dennis Msacky ni victim. Juhudi zozote zile za kutaka kumgeuza 'victim' kuwa mtuhumiwa lazima zitashindwa tu kwani siku zote HAKI hutamalaki.
Mtu yeyote anayetaka kutumia urafiki wangu na Dennis Msacky kutaka kujifurahisha kisiasa ajue kuwa furaha yake hiyo itakuwa ni ya muda mfupi sana maana ukweli ukidhihiri atapata aibu kubwa sana.

Ni muhimu sasa mambo haya tuiachie mahakama itende haki".