Ajira njiani: NUKUU 5 ZA NAIBU WAZIRI MALIASILI LAZARO NYALANDU BUNGENI MAY 2 2013


1. Tumeomba na tumeruhusiwa katika mwaka huu wa fedha tunaajiri vijana elfu moja waweze kuingia katika mapori yetu kama Maaskari wa Wanyama pori, tunaovijana wanaomaliza SUA, PASIANSI, Mwika na vyuo vingine wajiandae kwa sababu ajira inakuja kama mvua.
2. Hadi kufikia sasa hivi, tulikua na watu takribani mia nne (400) wanaofanya kazi kama Askari wa Wanyama pori katika Misitu yote Tanzania lakini idadi hii tutaiongeza, tunategemea kufikisha idadi ya Askari wa Wanyama pori elfu nne ili kuweza kufikisha kiwango kinachostahili kwa sababu sasa hivi Askari wetu mmoja analinda zaidi ya kilomita za mraba mia moja arobaini na saba ambazo kwa kweli kwa mtu mmoja ni ngumu sana.
3. Ni rahisi sana wakati mwingi kulaumu lakini mimi na Mheshimiwa Waziri tumeenda katika haya mapori tumekutana na hawa vijana, hali waliyonayo ikiwemo upungufu wa magari na vifaa ni mbaya… bajeti hiyo inaendelea kuandaliwa.
4. Tunaendelea kuinasa mitandao wanayoitumia kuwasiliana hawa Majangili ili kupanga mipango mbalimbali ya kufanya uhalifu, tunaendelea kufatilia usafirishaji kwenye bahari kuu.
5. Katika ziara yangu mimi binafsi nilipokua natembelea eneo la Serengeti, nilifika sehemu na kukuta Majangili wanne waliouwawa, inasikitisha lakini kazi ya kupambana na Majangili itaendelea.
Pia unaweza kumsikiliza Mbunge Felix Mkosamali (NCCR) akiongea bungeni kuhusu Wizara ya Mali Asili na Utalii pamoja na viongozi wa Serikali.