KABURI LA KANUMBA LAGEUZWA KITEGA UCHUMI, SASA UKITAKA KULIONA NI LAZIMA ULIPE TSHS 5,000/= KWANZA..!
02:48
KATIKA
kile kinachoonekana kwamba ni wizi mtupu, baadhi ya vijana wanaojifanya
kutunza Makaburi ya Kinondoni wamebuni njia ya kuwaibiawatu kwa kutumia
kaburi la nguli wa filamu za Kibongo, marehemu Steven Kanumba.Vijana
hao hujipatia kipato kwa kuwatoza watu wanaofika makaburini hapo
shilingi 5,000 kwa ajili ya kuliona na kupiga picha na kaburi la nguli
huyo. Utafiti uliofanywa na Risasi Jumamosi umebaini kwamba wageni
wanaotoka nje ya Dar ndiyo wanaoongoza kwa kulizwa zaidi.
Sosi wetu ambaye naye
alilizwa, alisema kuwa alishangazwa kwa kutozwa fedha na vijana hao
lakini hakuwa na budi kufanya hivyo yeye na wenzake ili kutimiza lengo
la kulitembelea kaburi hilo la kipenzi chao.
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili liliunda kikosi kazi cha waandishi wake na kwenda kuwanasa vijana hao.
WAANDISHI WATINGA MAKABURINI
Alhamisi
iliyopita, waandishi wetu walifika katika Makaburi ya Kinondoni na
kukutana na jamaa kibao waliokuwa wakijishughulisha na kazi za ujenzi wa
makaburi na kupanda maua ambapo walimchagua mmoja wao aliyejitambulisha
kwa jina la Mdenmark ili kuongea na wageni nao.
WAPANGA DAU
Baada ya
kuwaita chemba, jamaa huyo alianza kuwapiga somo waandishi wetu na
kuwaambia kwa kuwasaidia wampe shilingi 5,000 ili kuwaonesha kaburi na
kuwapa historia ya marehemu tangu enzi za uhai wake mpaka alipokutwa na
umauti huku akiwatahadharisha wafanye jambo hili kuwa siri.
MCHEZO WAMALIZWA
Baada ya
kukubaliana kiasi hicho cha fedha, waandishi walimpatia Mdenmark kiasi
cha fedha na akachukua jukumu la kuwapeleka mahali lilipo kaburi hilo.
Wakiwa kaburini kwa Kanumba, waandishi wetu kwa kutumia ustadi mkubwa
walifanikiwa kumpiga picha tapeli huyo akiwaelekeza mambo kadhaa juu ya
marehemu na picha nyingine zikimuonesha akipokea fedha kutoka kwa
waandishi.
TAMKO LA MHARIRI
Si sawa kulipa fedha kwa ajili ya kuliona kaburi la Kanumba, mara
kadhaa waandishi wetu wamemsikia mama mzazi wa marehemu Kanumba, Flora
Mtegoa akisema kuwa hafahamu mradi huo.
Ni jukumu la Jeshi la Polisi chini ya Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, DCP Suleiman Kova kuwanasa wajanja hao.
0 comments:
Post a Comment