Leo mahakamani "huku Lady JD na Ruge" Kule "Lwakatare na Kesi ya utekaji"
10:06
WAKATI
kesi ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare
ikitarajiwa kusikilizwa leo Mei 27 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Kesi ya msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya Judith Wambura (Lady
JayDee) pia inatarajia kusikilizwa tarehemu hiyo katika Mahakama ya
Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Lady JayDee anatarajia kupanda kizimbani kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhiwa hati ya mashtaka na kutakiwa kurudi mahakamani hapo kesho mei 27 .
Waandishi wa habari walishuhudia barua kutoka mahakamani hapo pamoja na nyakara zilizochapishwa na vyombo mbalimbali vya habari zikiwamo blogu zilizoelezea ugomvi wake kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Mkurugenzi wa Utafiti na Matukio Ruge Mutahaba.
“Hili
ndilo shtaka lenyewe kwa hivyo sisi hatuwezi kusema chochote kwa sasa
tunaelekea kwa mwanasheria wetu ili kuanza kuishughulikia kesi hii,”
alisema Gadna Habash mume wa mwanamuziki huyo.
Kabla
ya kufika mahakamani hapo mchana, mwanamuziki huyo alitoa mada katika
jukwaa la sanaa Basata ambako alizungumzia changamoto nyingi zilizopo
katika kufikia mafanikio kwenye sekta ya muziki.
Wakati
kesi hiyo inatarajiwa kuanza kusikilizwa Mei 27, siku nne baadaye
Jaydee anasherehekea miaka yake 13 tangu aingie rasmi katika sekta ya
muziki.
0 comments:
Post a Comment