Picha Mbali Mbali za eneo la tukio (Kanisa na waumini waliopigwa Bomu huko Arusha)
07:00Kwa sasa hali ya kawaida inaanza kurudi. Vyombo vya usalama vinaendelea kuchunguza ili kujua mlipuko huo ni nini hasa.
Balozi wa papa nchini na viongozi wa juu wa jimbo wameondoka eneo la tukio salama na balozi hajadhurika kabisa ingawa mlipuko huo ulilipuka karibu nao.
Mkuu wa mkoa alikuja na sasa ameondoka.
Wananchi wameanza kupungua eneo la tukio na wengi wanaelekea Mount Meru ili kuwatambua majeruhi. Hivyo idadi ya watu wanaondoka eneo la tukio na kwenda hospitali.
Polisi wamekamata pikipiki ambayo inasadikiwa imetumika katika tukio hilo.
Shughuli ya uzinduzi wa kanisa hilo imeahirishwa hadi tarehe ambayo haijatajwa
Mungu awajalie majeruhi wapate nafuu haraka.
0 comments:
Post a Comment