Habarini wana jf, kwa hali ya mambo
inayoendelea katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania, ni wazi
kuwa wabunge wengi wamepoteza sifa ya uwakilishi kwa wananchi katika
jengo lile la bunge mjini dodoma, wabunge wengi wameonekana kuwa
wasemaji wa serikali na si wa wananchi! Kufuatia hali hiyo kwa uchunguzi
wangu usio rasmi, nimegundua wako baadhi ya wabunge wachache bado wana
moyo wa uzalendo kwa wananchi na taifa lao kiujumla! Wafuatao ni wabunge
watano bora kwa uzalendo na utumishi uliotukuka kwa wananchi wao
waliowatuma bungeni:
1. Mh. Tundu Lissu(chadema)-singida mashariki.
2. Mh. John Mnyika(chadema)- Ubungo.
3. Mh. Deo Filikunjombe(ccm)-Ludewa
4. Mh. Kangi Lugora(ccm)-Mwibara.
5. Mh. Halima mdee(chadema)-kawe!
Pongezi
ziende kwa wananchi waliotuchagulia wabunge hao, pia pongeze ziende kwa
waheshimiwa wahusika! Mungu awalinde na kuwapa baraka zake!
Nawasilisha.
TOA MAONI YAKO HAPA
0 comments:
Post a Comment