Ushabiki: Afande Sele agoma kula siku 2 baada ya Simba kufungwa
09:54Akizungumza na Suddy Brown katika segment maarufu ya U Heard kupitia XXL ya Clouds FM, mke wa rapper huyo mkongwe Mama Tunda, amethibitisha kuwa mumewe amegoma kula toka siku ya mechi. Mbaya zaidi kwa Afande ni kuwa Mama Tunda na binti yao Tunda ni mashabiki wa Yanga hivyo wao na Selemani Msindi ni mashabiki wa timu mbili pinzani, hatupati picha humo ndani panavyokuwa ikifungwa timu anayoshabikia baba wa familia!. Minuno ya hatari bila shaka. Pole Afande.
0 comments:
Post a Comment