Lundenga amtimua mrembo jukwaani kwa kuvaa nusu utupu
09:15Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika Ukumbi wa Hoteli ya Kitalii ya Nashera mjini hapa wakati mrembo huyo alipokuwa akiwania kuvaa taji la mkoa huo.
Kisa cha mrembo huyo aliyevalia namba 5 kutimuliwa ni kukiuka maadili na kanuni za mashindano hayo kwa kuvaa nusu utupu mbele ya mgeni rasmi ambaye alikuwa Mbunge wa Kilosa, Mustapha Mkulo na mbele ya Kamati nzima ya Miss Tanzania.
Baada ya kuona jinsi alivyovaa, Lundenga na kamati yake walikubaliana kumtimua mshiriki huyo kwa kumwita Jaji Mkuu wa shindano, Alex Niktasi na kumtaka amuondoe haraka.
Mbali na Chumba, pia jaji alimtimu mrembo mwingine aliyevalia namba 8, Neema Joel (20) kutokana na kushiriki shindano hilo mara mbili mwaka huu, inadaiwa mara ya kwanza alishiriki mkoani Arusha.
Lundenga alipohojiwa na mwandishi wetu alisema kamati yake inataka kuendeleza nidhamu tangu ngazi ya chini, hivyo hawawezi kuruhusu utovu wa nidhamu.
0 comments:
Post a Comment