MLIE TUU ! WASTARA HATAOLEWA BONGO TENA
06:15Na Imelda Mtema
KAKA wa staa wa Filamu za Kibongo, Wastara Juma aitwaye Juma Juma ameliambia Risasi Mchanganyiko kwamba dada yake hatafunga tena ndoa nyingine hapa nchini.
“Iwapo dada yangu akitaka kuolewa atafanya hivyo Uarabuni siyo hapa kabisa,” alisema kaka huyo na kudai kuwa ameshuhudia mateso mengi ya dada yake kwa wanaume wa Kitanzania.
Kaka huyo amesisitiza kwamba wanaume wasipate tabu ya kumuuliza dada yake kuhusu suala la ndoa kwani watajisumbua bure.
Juma alizungumza kwa niaba ya dada yake ambaye awali alipigiwa simu ili kuulizwa kama alikuwa na mpango wa kufunga ndoa nyingine hapa nchini.
Hata hivyo, Wastara alimwachia kaka yake huyo kujibu badala yake, ingawaje kaka huyo hakufafanua kama dada yake ameshapata mtu wa kufunga naye ndoa huko Uarabuni.
Wastara alifunga ndoa tatu na wanaume tofauti na mume wake wa mwisho alikuwa msanii wa filamu, Juma Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia mapema mwaka huu.
Source:Global Publishers
0 comments:
Post a Comment