Breaking News: Lema Achiwa Huru
04:42Katika Mahakama hiyo kulikuwa na umati mkubwa wa wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Mashabiki, wafuasi na wanachama wa chama hicho walifurika katika mahakama hiyo kwa ajili ya kumuunga mkono mbunge
Hivi sasa mashabiki, wafurukutwa na wanachama wa Chadema wanafanya maandamano makubwa kuelekea katika ofisi za chama hicho ambazo zipo katika eneo la Ngarenaro.
Hivi sasa wanapita katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mulongo kwa maandamano huku wakipiga kelele za kusomea.
Kesi ya uchochezi dhidi ya Lema imefunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mkoa wa Arusha na endeshwa na Hakimu Devota Msoffe.
Mwandishi wa Habarimasai.com anasema kwamba kesi hiyo imeahirishwa mpaka Mei 29 mwaka huu.
Katika hati ya mashtaka ambayo ipo katika mahakama hiyo inasema kwamba kosa la Lema ni ' kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ni uchochezi. Endelea kusoma habarimasai. com kwa taarifa mbalimbali moto moto.
0 comments:
Post a Comment