Diamond – Wasanii tunanyonywa kwenye ringtone na makampuni ya simu
06:36
Jana kupitia Instagram, aliandika kilio chake:
Dah! hivi kweli Serikali imekosa
majibu ya swali la mh: Mbunge kuhusu mapato ya biashara ya ringtones..!?
Kweli sasa naanza kuamini kuwa Serikali Inatukumbatiaga tu kwa Mda
mfupi na kututumia Wasanii kwenye Kampeni zao kwa Maslahi yao Binafsi,
kisha wanatudump baada ya kufanikiwa kwenye uchaguzi wao, bila kujali
thamani na Mmhango wetu kwao.
Hata hivyo kuna watu wanaoamini kuwa
Diamond hapaswi kulalamika kwakuwa ndiye msanii anayefaidi zaidi matunda
ya muziki Tanzania.
Mmoja wa followers wake aitwaye
Princestepp aliandika: Hupaswi kulaumu wewe maanake kati ya wasanii
wachache walioweza kula hela za watanzania chini ya ya serikali ya rais
wetu Kikwete ni wewe acha unafiki wasanii wengine ambao hawajapata fursa
kama yako walaumu vipi sasa?
Diamond alijibu: Mi nimekula pesa na
bado nakula pesa kwa juhudi zangu za kujituma jukwaani na kufanya show
nzuri, sio kuwa naitwa kupewa pesa za ringtones nah! Napewa show…. So
nikiwa kama mfano mzuri kwa wasanii lazima niwe mstari wa mbele
kupigania haki za wasanii kiujumla.
Aliongeza, “Mi napigania haki zetu
upande mwingine wananiona snitch.. wakati mi naamini katika wasanii wote
japo nadhulumiwa lakini hakuna hata anayefikia hela nnayolipwa kwa
rintones.. ila naona haiwezekani kwanini watufanye wajinga watu wapewe
haki zao.”
0 comments:
Post a Comment