MTOTO AUAWA KIKATILI JIJINI MBEYA…..
05:57IMANI za kishirikina zimezidi kukitisa Kijiji cha Isange na Kata ya Isange baada ya matukio ya kupotea na kuawa kwa Watoto kutokea mara kwa mara ambapo Marehemu hukutwa wakiwa na mapungufu ya viungo ikiwemo Kichwa.
Katika tukio la hivi karibuni Mtoto mmoja aliyejulikana kwa Jina la
Lista Sebule (8) Mwanafunzi wa Darasa la Saba katika Shule ya Msingi
Mpombo iliyo katika Kata ya Isange Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya
Rungwe Mkoani hapa alipotea katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa
baada ya Siku 9 akiwa amekufa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo akiwemo Mama mzazi wa
Marehemu Christina Sakalile alisema binti yake alipotea majira ya saa
tisa jioni Machi 31, Mwaka huu baada ya kutumwa kupeleka simu kibandani
ili kuchaji lakini hakurudi hadi Saa Kumi na Mbili jioni hali iliyozua
wasiwasi na kuanza kumtafuta bila mafanikio.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa Kijijini ambapo
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Isange Daudi Nsyani ambaye baada ya kupewa
taarifa hizo pia aliwataarifu viongozi wa Kata akiwemo Diwani wa Kata ya
Isange Elias Mwasandele na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Brayson Nguro
ambaye aliitisha Mkutano wa wananchi.
Mtendaji huyo aliwaambia wananchi hao kushirikiana ili Mtoto
apatikane hali ambayoiliitikiwa na wananchi ambao walitaka Mtoto
apatikane aidha akiwa mzima ama Mfu ambapo juhudi za kumtafuta zilianza
na hatimaye kumpata Aprili 8, Mwaka huu akiwa amekufa huku akiwa hana
baadhi ya Viungo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mwili wa Marehemu ulipatikana
ukiwa pembezoni ya Mto Nkalisi uliopo Kijijini hapo ukiwa umenyofolewa
baadhi ya viungo kama Kichwa na Miguu ambapo mguu mmoja ulipatikana
baada ya Mbwa kukutwa akiwa ameshika na kuudondosha baada ya kukutana na
watu hali iliyowalazimu watu hao kumfutilia Mbwa huyo aliyeongoza hadi
Mwili wa Marehemu ulipokuwepo na kuwakuta Mbwa wengine wawili wakiwa
pembezoni.
Baada ya kupatikana kwa mwili huo Taarifa ilipelekwa Polisi ambao
walifika katika eneo la tukio na kuupima kisha kuwakabidhi ndugu kwa
ajili ya mazishi ambapo watu wawili walikamatwa kuhusika na tukio hilo
baada ya kupigiwa kura za siri na wananchi na kukutwa na kura nyingi
ambapo wengine wanne waliachiwa kutokana na kutokuwa na kura nyingi.
0 comments:
Post a Comment