Kama ulikuwa mshabiki wa mambo ya Bungeni hivi ndivyo ilivyo.


KAMA hujui ndiyo ujue sasa, kwamba waheshimiwa wetu wanapokuwa ndani ya mjengo na kutoleana maneno machafu na yenye vitisho unaweza kusema nje watanuniana au hata kupigana singi, lakini waapi! Gelesha tu.

Baadhi ya wananchi wanaohudhuria vikao vya bunge mjini hapa wanasema wabunge hao, hasa wa Chadema na CCM wanapokuwa ndani ya mjengo ni maadui wakubwa, wakahoji:

Lakini mbona wakitoka nje wanachekeana sana, tena marafiki au wanatuzuga wapiga kura wao tuwaone wako siriasi?”

Mmoja akaendelea: ”Mimi naamini kwamba wanapokuwa nje ya bunge ni marafiki na wanapokuwa mjengoni wanachofanya ni kulinda itikadi zao za kisiasa tu, hakuna lingine.”

Akaendelea kuwa, wananchi wengi huamini kwamba waheshimiwa ni maadui wa moja kwa moja, hasa…