Mshtuko wa bomoa bomoa

MAGHOROFA yaliyojengwa kandokando ya Mto Mlalakua na Ufukweni mwa Bahari ya Hindi yatabomolewa, hivyo kuzua mshtuko mkubwa kwa wamiliki.
Uchunguzi  uliofanywa na gazeti hili kwa zaidi ya wiki nne umebaini kwamba kazi ya kubomoa nyumba hizo inaweza kuanza wakati wowote ingawa kuna changamoto kubwa kwani baadhi ya nyumba hizo ni za vigogo wenye madaraka makubwa serikalini au ndani ya vyama vya siasa.

Habari zaidi zinadai kwamba baadhi ya vigogo hao wamekimbilia mahakamani kufungua  kesi ya kupinga nyumba zao zisiguswe wakati wengine wamekua wakitoa vitisho kwa waliopewa…