Mama Mwizi



Mama mmoja ambaye ni maarufu kwa wizi wa simu kwenye sherehe mbalimbali alitoa kali ya mwaka alipofumwa akiiba simu kwa kuvua nguo zake zote na kubakia uchi wa mnyama ili kuthibitisha hajaiba simu. Mama mmoja ambaye ni miongoni mwa wanawake wanaotafutwa kila siku kwa wizi wa simu kwenye harusi na sherehe mbalimbali, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kukamatwa katika ukumbi wa Delux uliopo Sinza Kijiweni.

Mama huyo amekuwa na tabia ya kujifanya ni miongoni mwa waalikwa kumbe siyo ni mtaalamu wa kuiba simu za watu katika sherehe.

Jumamosi iliyopita aliingia katika ukumbi wa Delux katika harusi ya mmoja wa wafanyabiashara katika maduka ya Kariakoo, aliyefahamika kwa jina la Alexander na mkewe Augustina na kuwa mmoja wa wageni waalikwa kumbe alikuwa na nia ya kukusanya simu za watu.

Harusi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mc Kibonde ambaye ni mtangazaji wa Redio Cluods ilikuwa ya kufa mtu kwani kila aina ya vinywaji vilikuwepo na akina dada wenye kujishebedua walikuwa na mahala yao.