Mbowe awapongeza wabunge wa CCM kwa msimamo


Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amepongeza msimamo wa wabunge hasa wa CCM kwa kuweka itikadi zao pembeni na kusimamia kidete suala la bajeti ya Wizara ya Maji, hadi ikasitishwa ili iboreshwe zaidi. Pia kiongozi huyo, pamoja na kudai kuwa adhabu waliyopewa wabunge watano wa chama chake haikustahili, lakini akakiri kuwa walihusika katika vurugu ndani ya Bunge, ikiwa ni pamoja na mmoja wao kudharau mamlaka ya Spika.
Aidha, Mbowe amebainisha kuwa kambi ya upinzani inataka utaratibu wa mashine za kupigia kura zilizopo ukumbini kwenye kila meza ya mbunge uanze kutumika mara moja, badala ya kura za ndiyo na hapana ili kuondokana na mikanganyiko na kutotendeka kwa haki wakati wa..read more
habarileo