Nimeiona orodha ya nchi 20 masikini
zaidi dunia na jambo la kufurahisha ni kuwa tanzania haipo kwenye
orodha hiyo.nchi ya msumbiji ipo kwenye orodha ya nchi masikini lakini
kuna jambo limenishangaza kidogo.thamani ya pesa ya msumbiji iko juu
zaidi na ya kwetu kwa maana kwasasahivi 1000tsh = 18.97 meticais.sasa
wale ndugu zangu wataalamu wa uchumi naomba mnisaidie kuhusu hili.kwa
upeo wangu mdogo thamani ya pesa ya nchi fulani yaweza kutumika kama
kigezo cha kubaini hali na kiwango cha uchumi wa nchi fulani?najua zipo
sababu zingine kadhaa lakini hili limenishangaza kwa kiasi fulani
Read more Here:
http://www.therichest.org/world/poorest-countries-in-the-world/
TOA MAONI YAKO HAPA
0 comments:
Post a Comment