LAURYN HILL MATATANI KUFUNGWA

Huenda mwanamuziki Lauryn Hill akafungwa baada ya kukwepa kulipa kodi ya zaidi ya dola 554,000 ambazo aliahidi kulipa

Hill alistakiwa baada ya kushindwa kulipa kudi ya pango ambapo aliahidi kuwa angezilipa kabla ya kutolewa kwa hukumu ya kesi hiyo ambayo ilikuwa itolewe wiki hii lakini ikahairishwa hadi Mei  6 mwaka huu

Wakati wa kuhairisha kwa hukumu hiyo hakimu wa jimbo la New Jersey, Madeline Cox alisema kuwa mwanamuziki huyo haonyshi jitihada za kulipa deni hilo hivyo kinachofuatia ni hukumu dhidi yake kwa kuwa hilo ni kosa la jinai