Mtwara yachafuka

Hali ya usalama katika mji wa Mtwara toka jana asubuhi imekuwa ni tete. Hakuna mabasi yanayoingia na kutoka katika mji huo toka asubuhi, kuna baadhi ya mitaa matairi yamechomwa moto barabarani, magari ya FFU yametanda kila kona za mji. Habari zilizotufikia hivi punde zimeeleza kuwa kwa sasa hakuna  mawasiliano ya televisheni ya Taifa TBC, milio ya mabomu inasikika kila kona na hali ya utulivu sio ya kuridhisha, Askari wa zima moto wamesambaa kuzima moto na kuna baadhi ya nyumba maeneno ya Shangani zimechoma moto....

Kauli mbiu ya Mtwara sasa - "GESI HAITOKI HATA KWA BOMBA LA PENI"
 
Source: Chinga one blog