Wassira amtaka Sitta "kujiuzuru".

Wassira amemwambia Sitta "kama unaona serikali inaendeshwa kwa rushwa jiuzuru", akaendelea kusisitiza, "huwezi kuwa kwenye serikali hiyo hiyo bado unaisema ni serikali ya kifisadi wakati na wewe ni sehemu ya serikali."

Wassira pia aliongeza yafuatayo, "huwezi kuisema serikali vibaya wakati na wewe ni sehemu ya serikali hiyo, vinginevyo ndugu Sitta aachie ngazi la sivyo huu utakuwa utapeli wa kisiasa".

Aidha, katika kuimalizia hoja yake hii aliuliza swali, "samaki mmoja akioza, wote wanaoza, sasa yeye (akimaanisha Sitta) atasalimika vipi?"

My take;

Mhe. Sitta nadhani ana hitaji kukopeshwa busara kidogo, katika hatua hii huwezi kujifanya una chukizwa na madudu ya serikali ambayo kwa kipindi chote hiki amekuwa akiitumikia, amekuwa sehemu ya serikali hiyo na kama akisema kuna madudu, na yeye tuseme ni miongoni mwa wazalisha madudu hayo.

Mhe. Sitta, kiu ya urais isikufanye uonekane kituko mbele ya watanzania, kuwa mpole na usubiri wakati muafaka, kwani tabia hizi za kuropoka ropoka ndani ya CCM hatunazo, tuwaachie hii tabia wasaka dola bila mbinu (CHADEMA).
TOA MAONI YAKO HAPA