Diwani Arusha asimulia alivyolipuliwa na bomu
00:55Arusha.Diwani wa Chadema Kata ya Kiranyi wilayani Arumeru mkoani Arusha,Patrick Bille ameeleza kwa masikitiko jinsi bomu lilivyomlipua na kusema kwamba awali akiwa karibu na jukwaa kuu aliona mfuko wa plastiki ukipepea angani ambao ulitua chini ya jukwaa na kisha kulipuka.
Bille ambaye kwa sasa anaishi akiwa na vipande vya chuma mwilini alisema kuwa,kabla ya mfuko huo kutua ardhini alifikiri ni jiwe kwa kuwa alikuwa mita tatu tu kutoka ulipotua lakini ghafla alishangaa kuona ukilipuka na kumjeruhi vibaya.
“Wakati nikiwa pale jukwaani niliona mfuko mweusi ukipepea angani nikahisi ni jiwe limerushwa ghafla ulitua karibu na nilipokuwa lakini nikasikia mlipuko ghafla na kuna vyuma vikanirukia ,”alisimulia Bille.
Hata hivyo,alisema kuwa hakumwona mtu aliyerusha mfuko huo lakini ulitokea upande wa Baa ya Soweto iliyokuwa mkabala na jukwaa kuu upande wa Magharibi.
Akiendelea kusimulia alisema kwamba mara baada ya mfuko huo kulipuka alipigwa na vipande vya chuma katika eneo la kifua chake na mkono wa kulia na kisha kupoteza fahamu na kujikuta akiwa hospitali ya Selian.
Hata hivyo,alisema kuwa anakumbuka wakati akiwa jukwaani kulikuwa na amani ya kutosha na neno la mwisho analolikumbuka lilitamkwa na Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe ambapo aliwataka watu wakichangie chama chao fedha za kuwawezesha kumaliza uchaguzi salama.
“Pale jukwaani nakumbuka kulikuwa na amani kabisa lakini nakumbuka neno la mwisho alilosema mwenyekiti wangu kwamba watu wachangie fedha za kukisaidia chama kishinde uchaguzi,”alisisitiza Bille
Diwani huyo kwa unyonge alisema kuwa baaya kufikishwa hospitalini hapo madaktari walimwambia ya kwamba ameonekana na vipande vya chuma mwilini ambavyo vimeingia umbali wa inchi mbili na wanasubiria visogee ili viweze kutolewa.
0 comments:
Post a Comment