STEVE NYERERE: NATESEKA NA UGONJWA
10:02“Mkono umevimba, unatoa majimaji kama vile nimeungua na moto na mifupa inaniuma sana kiasi cha kushindwa kufanya shughuli zangu,” alisema.
Staa huyo alimwambia mwandishi wetu kwamba chanzo cha ugonjwa huo ni maralia iliyompata na kwenda hospitali ambako aliandikiwa dawa mseto.
“Nilitumia dozi ya kwanza, kisha ya pili hapo ndipo tatizo lilipoanza, hospitali wanasema nina aleji,” alisema.
Hali hiyo imemfanya Steve kudhoofu na muda mwingi kushinda ndani kwa takribani wiki mbili sasa kwa kuwa mifupa ya mkono huo inamuuma sana hususan usiku unapoingia.
Aidha, Steve amewashukuru mastaa wenzake wanaompa sapoti kwa kumtembelea na kumjulia hali na akawataja wachache kuwa, ni Jacob Steven ‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’ Mama Rolaa na Sabrina Rupia ‘Cathy’.
0 comments:
Post a Comment