ABIRIA 60 WANUSURIKA KUFA BAADA YA BASI LA TURU KUCHOMWA MOTO NA WANAKIJIJI HUKO SINGIDA.

Abiria wapatao 60 waliokuwa wanasafiri na basi la Turu linalofanya safari zake kati ya mkoa wa Singida na Haidom mkoani Manyara, wamelazimishwa kuteremka toka ndani ya basi hilo na wananchi zaidi ya mia mbili ( 200 ) wa vijiji vitatu, na kisha kulichoma moto basi hilo.


Taarifa toka eneo la tukio zinasema wananchi hao ni wa vijiji vya Singa, Idabagadu na Nkungi mkoani Singida, ambao baada ya kuhakikisha abiria wote wameshuka, walilichoma moto basi hilo ambalo limetekea sehemu kubwa.


Sababu ya wananchi hao kuchukua uamuzi huo ni kutokana na basi hilo kumgonga mwanakijiji mmoja na kufa wiki tatu zilizopita