Babuu Sambeke afariki dunia jana kwa ajali ya ndege ya marehemu Advocate Mawalla.
07:31Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba ndege iliyokuwa inamilikiwa na Wakili maarufu Marehemu Nyaga Mawala aliyefariki wiki 3 zilizopita na kuzikwa huko Nairobi imeanguka ikiwa katika hatua za mwisho za kutua (final approach) katika kiwanja cha ndege cha arusha.
Taarifa zinasema kuwa ndege hiyo ilikuwa na rubani pekee anayejulikana kwa jina Babu Sambeke, au maarufu kama Bob Sambeke aliyekuwa anatokea West Kilimanjaro.
Taarifa zaidi zinasema kuwa hali ya rubani huyo si nzuri sana, na amekimbizwa kwenye hospitali ya Mount Meru kwa matibabu.
Maelezo zaidi kuhusu ajali hiyo ni kwamba ndege hiyo ilijaribu kutua baada ya masaa ya kawaida ya kufunga kiwanja(saa 12.30jioni) kupita.
UPDATE:
BOB SAMBEKE ALIYEKUWA RUBANI WA MAREHEMU WAKILI MAWALA. NYAGA NAYE KAFARIKI DUNIA MUDA MFUPI BAADA YA KUFIKISHWA HOSPITALI YA MOUNT MERU.
0 comments:
Post a Comment