HIZI NDIZO SABABU KUU ZA WANAWAKE WENGI KUVAA NUSU UCHI
23:12
Wakati mwingne wanaume au watu tofauti hudhani kwamba, wanawake
wanaovaa nusu uchi huwa wanafanya hivyo kwa sababu ya kutafuta soko kwa
wanaume.
Inawezekana kukawa na wale ambao wana sababu hizo, lakini wapo
wale ambao wanalipa fidia kutokana na kuamini kwao kwamba wanamapungufu
kwa mfano sura zao zimewaangusha, hivyo miguu yao mizuri inabidi kuziba
pengo au udhaifu huo.
Wakati mwingine hata wanawake wanaodhani au kudhaniwa kuwa ni
wazuri, wamekuwa wakivaa nguo fupi zinazoonyesha maungo yao.Hawa nao ni
lazima wanalipa fidia ya kasoro fulani waliyo nayo.
Inawezekana wameshindwa kulinda ndoa zao, au inawezekana
hawajaolewa na sasa wanataka kuonyesha kwamba, pamoja na kutoolewa kwao,
bado wao wana sura na miguu au miili mizuri.Udhaifu wowote ambao unamkera mwanamke iwe ni wa moja kwa moja au kupitia nyuma ya ubongo wake, unaweza kuonyeshwa kwa mwanamke huyo kuyatangaza yale maeneo ya mwili wake ambayo anaamini ni mazuri.
Kuyatangaza huko humpa ahueni kwa kuamini kwamba bado anayo
thamani, kwani ataangaliwa sana na wanaume, kusifiwa na pengine
kutongozwa.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya.
Hebu angalia wanawake ambao wanavaa nguo za kubana huku wakiwa na makalio makubwa. Hawa mara nyingi wana sura ambazo wao au wengi huamini kwamba ni mbaya.
Huvaa nguo hizi ili kuonyesha kwamba, pamoja na ubaya wa sura zao,
bado wao ni wazuri sana katika maeneo mengine ya mwili ambayo wanaume na
hata wanawake wengi huyapenda au kutamani kuwa nayo.
Wengi hawavai tu nguo hizi za kubana kwa sababu ni fasheni, la hasha, wengi hili ni kimbilio la udhaifu wao
0 comments:
Post a Comment