MIAKA 13 YA LADY JD KATIKA MUZIKI KUAMBATANA NA ALBAMU MPYA YA 6


Nashukuru vyombo vyote vya habari vinavyoshiriki kikamilifu kukuza na kulinda sanaa ya muziki Tanzania bila kujali maslahi binafsi...Tumeandaa sherehe kubwa na nzuri ya miaka 13 ya LADY JAYDEE katika muziki. Sherehe ya miaka 13 ya Lady JayDee katika muziki itaambatana na uzinduzi wa album yangu ya sita inayokwenda kwa jina la ‘NOTHING BUT THE TRUTH’ ambayo ina jumla ya nyimbo 10.
Katika sherehe hizo pia kutakuwa na show ya nyimbo zote bora za JayDee nikishirikiana na baadhi ya wasanii wenzangu hapa nchini.Sherehe zitafanyika Ijumaa tarehe 31 May 2013.
Nawakaribisha wote tufurahi pamoja
Na Mungu Awabariki
 
TOA MAONI