Mambo ya Anti Ezekiel.......................... Paukwa?

Kweli sikio la kufa halisikii dawa! Licha kuolewa na Sunday Demonte, msanii wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel ametia aibu kwa mara nyingine tena baada ya kunaswa nusu utupu ukumbini usiku wa manane, Risasi Jumamosi linafunguka.


Baada ya midume kumuona akiwa amevaa kihasara huku akijificha nyuma ya jukwaa baadhi yao walimfuata na kuanza kumzingira kisha kumwagizia ulabu kama mvua kila mmoja akitamani kuondoka naye kwenda kumfaidi kimapenzi.
Baadhi ya madalali wa magari wa eneo la Masika mjini hapa walimvamia Aunt na kuanza kumgombea wakiongozwa na mmoja wao aliyeonekana kuwa jirani zaidi na msanii huyo.

Mwanahabari wetu alipomfuata Aunt na kumuuliza kulikoni akatoka Dar kuwafuata Ngwasuma Mji Kasoro Bahari huku akiwa kihasara kiasi hicho, mke huyo wa mtu alifunguka: “Nipo hapa Moro zaidi ya siku sita na nitaendela kuwepo kwa zaidi ya siku kumi, nipo na kundi langu tunarekodi filamu kwenye Hoteli ya Nashera.”

Alipobanwa kuhusiana na kinguo alichovaa huku mapaja na maungo mengine nyeti yakionekana, alicheka na kukatisha mahojiano: “Siwezi kuzungumza chochote kama vipi chukua namba yangu unipigie kesho.”
Kesho yake alipopigiwa, simu yake iliita bila kupokelewa.
Siyo mara ya kwanza, Aunt amekuwa akifanya matukio yasiyoendana na hadhi ya mke wa mtu akijiachia kihasara ikiaminika kuwa anafanya hivyo kwa kuwa hakai na mumewe ambaye yupo huko Dubai.