WANAFUNZI 20 WA CHEKECHEA WANUSURIKA KATIKA AJALI ...
11:28
Ajali hiyo imetokea jana mchana katika eneo la Msikiti wa Hidaya katika kata ya Mvinjeni katikati ya mji wa Iringa.
Walioshuhudia tukio hilo wamesema daladala hilo lilikuwa likitokea
eneo la FRELIMO katika Manispaa ya Iringa kuelekea mjini Iringa na baada
ya kufika eneo hilo lilishindwa kupanda mlima na kuanza kurudi nyuma
kwa kasi kabla ya kupinduka.
Alisema shuhuda, Juma Omari kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa
dereva ambaye alionekana kuendesha gari hilo kwa bila kuchukua tahadhari
pamoja na kutambua kuwa mbele kuna kona na mlima.
Anasema, wananchi walitoa msaada wa kuwatoa katika daladala na kuwakimbiza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa.
Katika ajali hiyo hakuna aliyepoteza maisha zaidi ya mwanamke
mmoja ambae jina lake bado kufahamika aliyejeruhiwa vibaya mikono yake.
Mmoja kati ya wauguzi wa Hospitali ya mkoa wa Iringa ambae hakutaka
kutaja jina lake kwa kuwa si msemaji wa Hospitali hiyo alisema kuwa hali
za watoto hao si mbaya sana zaidi ya kupata michubuko midogo midogo.
0 comments:
Post a Comment