Maalim Seif: Nitaomba kuwania tena urais mwaka 2015
22:23
Makamu wa
Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad amesema ataomba
tena kugombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) katika Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2015. Akizungumza
katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha runinga cha
ITV, Maalim Seif alisema kuwa anachoomba tu Mwenyezi Mungu ampe afya
njema. “Ni
uamuzi wa wananchi na wanachama wenyewe wa CUF lakini kama Mwenyezi
Mungu akinipa afya na uzima bado nia ipo,” alisema Seif ambaye pia ni
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Alisema
hivi sasa chama hicho kimekuwa kikijiimarisha visiwani huko kwa kufanya
mikutano Pemba na Unguja ili kuhakikisha kinaendelea kukubalika kwa
wananchi.
Kauli hiyo
ya Maalim Seif ambaye amekuwa akiwania nafasi hiyo tangu kuingia kwa
mfumo wa vyama vingi, ilipokewa kwa hisia tofauti ambapo Mhadhiri wa
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bashiru Ali alisema vyama vya siasa ni
lazima viwe vinatayarisha viongozi wa baadaye ambao watafahamu kwamba
uongozi ni dhamana wanayopewa na wananchi.
Naibu Katibu
Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema Maalim Seif kama mwanachama wa
chama hicho anaruhusiwa kwa mujibu wa Katiba kugombea nafasi yoyote ya
uongozi wa dola.
Chanzo - Mwananchi
Picha - ChingaOne blog Library
0 comments:
Post a Comment